Wakuu wa Nigeria wanasema kuwa wamevamia mara kadha nyumba za mshauri wa usalama wa zamani.
Idara
ya usalama wa taifa imesema kuwa uvamizi huo umefanywa kufuatana na
taarifa za upelelezi za kuaminika, zilizomhusisha Mohammed Sambo Dasuki
na mipango ya kufanya uhalifu dhidi ya taifa.
Ilisema kuwa bunduki na zana nyengine za kijeshi zilikutikana kwenye nyumba hizo zilizovamiwa.
Bwana Dasuki alitolewa juma lilopita katika kazi yake ya kuishauri serikali kuhusu usalama
