
Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre
atafikishwa mahakamani nchini Senegal kwa makosa ya uhalifu dhidi ya
binadamu, ukatili dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita .
Kesi hiyo mjini Dakar ni ya kwanza ya aina yake ambapo nchi moja ya Afrika imemshitaki kiongozi wa zamani wa taifa jingine.
Bwana
Habre anashutumiwa kwa kuhusika na vitedo vya ukatili na mauaji ya
maelfu ya watu wakati wa enzi ya utawala wake kuanzia 1982 hadi 1990,
shutuma anazozikanusha..
Kesi hiyo inafuatia miaka 25 ya kampeni za kumfikisha mbele ya sheria.
Wengi miongoni mwa watu wanaodaiwa kuwa waathirika wa uhalifu
uliotekelezwa na Bwana Habre' wamekua wakitoa wito wa kufunguliwa
mashtaka dhidi yake tangu alipopinduliwa mamlakani na kukimbilia
uhamisho nchini Senegal 1990.
Mnamo mwaka 2005 mahakama ya
Ubelgiji iliytoa kibali cha kumkamata, ikidai kuwa na haki ya kimataifa
ya kufanya hivyo , lakini baada ya mazungumzo na Umoja wa Afrika , AU
iliiomba Senegal kuendesha kesi dhidi Bwana Habre " kwa niaba ya Afrika
".