Rais wa Ufaransa, Francois Hollande,
ametaka kuundwe serikali kamili ya Ukanda wa Ulaya, itakayokuwa na
bunge lake na bajeti yake nzima. Katika mahojiano na gazeti moja la
nchini Ufaransa, bwana Hollande amesema kuwa mkasa ulioikumba Ugiriki ni
ishara tosha kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi kati ya nchi wanachama
wa Ulaya na hata utumiaji wa sarafu moja.
Huku hayo yakitokea,
nchini Ujerumani, Chansela Angela Merkel ameambia vyombo vya habari kuwa
yuko tayari kujadili uwezekano wa kusamehe sehemu ya deni la Ugiriki,
lakini kwa sharti kuwa maelezo yote yakamilishwe katika makubaliano ya
punde zaidi ya kuukomboa uchumi wake kupitia deni lipya.
Hatma ya Mabenki
Hii leo mabenki ya Ugiriki yanatarajiwa kufunguliwa baada ya kufungwa kwa wiki 3.
Mabenki
hayo hata hivyo yanafunguliwa huku kkodi inayotozwa kwa bidhaa muhimu
ikipandishwa ikiwemo pia kwa mahoteli na sekta nzima ya usafiri. hatua
hii inanuiwa kurejesha imani a raia wa ndani ya Ugiriki na hata jamii ya
kimataifa nje ya Ugiriki kufuatia msaada uliokuja kwa masharti ya
kufanywa mageuzi kusainiwa wiki iliyopita na hivyo kukomboa nchi hiyo
isifilisike.
Bado idadi ya juu zaidi ambayo raia wataruhusiwa
kutoa kwenye akaunti zai itaendelea kudhibitiwa na benki kuu ya nchi.
awali idadi hiyo iliwekwa kuwa Euro 60 kwa siku, japo sasa kuna
matumaini idadi hiyo ikaongezwa hadi Euro 240 kwa siku. hata hivyo wengi
wa raia wanasema kuwa kwa muda mrefu uchumi wa nchi hiyo umeharibika na
wameshazoea kuishi kwa hata chini ya idadi hiyo kwa siku.