
Mazungumzo ya mwisho ya kuzima msukosuko wa kisiasa wa Burundi, yamesimamishwa, siku mbili kabla ya uchaguzi wa rais.
Waziri
wa mambo ya ndani wa Burundi, ameripotiwa akisema, kuwa mpatanishi
mkuu, yaani Uganda, imeombwa iruhusu mazungumzo yasimamishwe baina ya
serikali ya Burundi na vyama vya upinzani.
Pande zote mbili zinalaumiana kwamba hazionyeshi nia njema kwenye mazungumzo.
Upinzani
umesema utasusia uchaguzi huo, ambapo rais Pierre Nkurunziza anawania
muhula wa tatu hatua ambayo inaonekana na wengi kuwa kinyume na katiba.
Hatua hiyo ilizua maandamano ya majuma kadhaa na jaribio la mapinduzi awali mwaka huu.