
Watu watano miongoni mwao maafisa
wawili wa polisi wamefariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria
kukanyaga bomu la kutegwa ardhini.
Watano hao walikua wakielekea mjini Lamu katika Pwani ya Kenya
Kamishna wa jimbo la Garisa anasema kuwa maafisa hao walikuwa kazini wakielekea eneo la Hindi, kununua bidhaa za matumizi.
Mwandishi wa BBC aliyeko Garissa anasema kuwa gari hilo la serikali
liliharibiwa vibaya katika shambulizi hilo la kwanza la aina hiyo.
Alisema kuwa bomu hilo lilikuwa limetegwa barabarani.
Uchunguzi wa kwanza unaashiria kuwa hilo lilikuwa ni shambulizi la kundi la wapiganaji wa kiislamu kutoka Somalia Al Shabaab.
Mwezi uliopita jaribio la wanamgambo hao kuishambulia kambi ya jeshi la Kenya katika eneo hilo lilipelekea 11 kati yao kuuawa.
Hiyo
ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa wapiganaji wa kigeni kupatikana
miongoni mwa washambulizi wa kundi hilo baada ya mwili wa muingereza
Thomas Evans ulipatikana.