
Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa
makubaliano ya kihistoria yametangazwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran
na mataifa 6 makubwa duniani.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Iran
na mataifa sita zenye nguvu duniani wanakutana kwa mara ya mwisho huko
Vienna baada ya makubaliano rasmi kutatangazwa katika mkutano na
waandishi habari.
Balozi wa maswala ya kigeni wa bara Ulaya Federica Mogherini,
amechapisha mwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa makubaliano
kuhusiana na mradi wa kinyunklia wa Iran yameafikiwa.
Bi Mogherini
amesema kuwa ni wazi mazungumzo ya kidiplomasia yanaweza kuleta
mabadiliko makubwa ya sera kushinda makabiliano ya kijeshi ya miongo
kadhaa.
Rais wa Iran , Hassan Rouhani, amesema kuwa majadiliano hayo yamekuwa na ufanisi mkubwa.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya kidiplomasia aliyeko mjini Vienna
anasema kuwa licha ya matokeo ya mazungumzo hayo kutojulikana inaonekana
kuwa iran imekubali uchunguzi wa umoja wa mataifa kukagua mipango yake
ya nyuklia.
Makabuliano hayo pia yanatarajiwa kutoa ratiba ya kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa ilivyowekewa Iran.
Mkuu wa shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia duniani ametoa maelezo kuhusu makubaliano yaliyoafikiwa.
Yukiya Amano amesema kuwa ''Iran imetia sahihi mpango wa kufafanua masuala yenye utata.''
Amano alisema kuwa anatarajia ukaguzi ulio kamili kwa mipango ya nyuklia nchini Iran ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Akitoa maoni yake kuhusu makubaliano hayo waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameyataja kuwa ''makosa ya kihistoria''.