
Nyumba ya nyota wa muziki Chris
Brown kutoka Marekani imevamiwa na kupekuliwa na watu watatu waliofunika
nyuso zao ambao walimfungia shangazi lake ndani chumba chake kulingana
na maafisa wa polisi.
Nyota huyo wa muziki wa R&B hakuwepo nyumbani kwake wakati wa wizi huo ambao ulifanyika alfajiri siku ya jumatano.
Maafisa
wanasema kuwa washukiwa ambao walikuwa na bunduki waliondoka katika
jumba hilo la Tarzana na fedha za kiasi kisichojulikana pamoja na vitu
kadhaa vya kibinafsi.
Brown au wawakilishi wake bado hawajatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.
Kulingana na ripoti,nyota huyo alikuwa ameenda kujivinjari katika kilabu moja wakati wa kisa hicho
Hii
ni mara ya pili ya nyumba ya msanii huyo ambaye alikuwa mpenziwe nyota
wa muziki wa Pop Rihanna kuvamiwa katika kipindi cha miezi ya hivi
karibuni.
Mnamo mwezi Mei,aliwasili nyumbani na kumpata mwanamke
mmoja aliyedaiwa kuvunja na kuingia kupika vyakula kadhaa na kuandika
ukutani kwamba anampenda msanii huyo.