
Shirika la fedha duniani IMF
limelaumu vikali masharti ya msaada wa kifedha ambao linasema mataifa
yanayotumia sarafu ya euro yaliipa Ugiriki.
Afisa mmoja wa IMF
amesema kuwa mabadiliko hayo ya Ugikiri ni vigumu kutekeleza na malengo
katika ukuaji wake yatakuwa magumu kutimizwa.
IMF inasema kuwa Ugiriki inaweza kustahimili deni lake kwa kuchukuliwa hatua ambazo Ulaya haijakuwa na nia kuzitekeleza.
Waziri mkuu wa ugiriki Alexis Tsipras amekuwa akijaribu kuwashawishi
wabunge kuyaunga mkono mabadiliki yaliyotolewa na mkutano wa Brussels
huku yeye mwenyewe akisema kuwa hana imani nayo.
Kwenye mahojiano
na kituo kimoja cha televisheni bwana Tsipras alisema kuwa Ugiriki
ingetimiliwa kutoka kwa muungano wa Ulaya ikiwa haingekubali makubaliano
hayo.