
Ni kesi iliodumu takribani
miaka saba na kuziteka hisia za wananchi wengi wa Tanzania kwani ilikuwa
ikiwahusisha viongozi wa ngazi za juu serikalini kwa kashfa ya kutoa
msamaha wa kodi kwa kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza bila
kufuata kanuni.
Mawaziri hao wamepelekwa katika gereza la Keko jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa
waziri wa fedha Bazil Mramba akatiwa hatiani katika mashitaka yote 11
yaliyokuwa yakimkabili ambapo mashitaka 10 yalikuwa ni ya matumizi
mabaya ya madaraka na shitaka la 11 likiwa ni kuisababishia serikali
hasara ya shilingi bilioni 11. 7 sawa na takribani dola elfu tano za
Marekani.
Daniel Yona aliyepata kuwa Waziri wa nishati na Madini,
naye akitiwa hatiani kwa makosa matano ya matumizi mabaya ya madaraka na
kuisababishia hasara serikali.
Mshitakiwa mwingine wa tatu ambaye
alikuwa katibu Mkuu wa zamani wa wizara ya fedha ya Tanzania, Aggrey
Mgonja aliachiwa huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa
kuthibitisha mashtaka yote 11 yaliyokuwa yakimkabili.