
Kundi la kutetea haki la Global
Witness limayalaumu baadhi ya makumpuni ya mbao barani Ulaya kwa
kusaidia kufadhili vita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kupitia
kusaidia kusaini mikataba ya fedha nyingi na makundi ya wapiganaji.
Kundi hilo la Global Witness pia linasema kuwa muungano wa Ulaya umeshindwa kuzuia mbao haramu ambazo zinauzwa barani Ulaya.
Maelfu
ya watu wameuawa miaka ya hivi majuzi nchini Jamhuri ya Afrika ya kati
kwenye mzozo ambao ulisababisha kuwepo kwa mauaji ya waislamu ambao ni
wachache nchini humo.