Serikali ya Ugiriki iko mbioni
kuandika mapendekezo mapya yatakayo kwamua mazungumzo ya kutafutia
ufumbuzi wa matatizo yake ya kiuchumi.
Hii inafuatia muda wa siku tano uliotolewa na viongozi wa Ukanda wa Ulaya mjini Brussels kwa nchi hiyo kuleta mapendekezo yake.Kauli hiyo ya waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras inafuatia tamko la Rais wa Baraza la Ulaya Donuld Tusk kwa bunge la Ulaya.
Akizungumzo wakati wa mkutano na viongozi wa ukanda wa Ulaya, bwana Tusk amesema uwa huu ndio wakati mgumu zaidi kwa bara ulaya.
Ugiriki imepewa hadi Ijumaa , siku ya mwisho ya kuwasilisha mapendekezo yake ya kukwamua uchumi wake.
Kwa upande wake rais wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, ametahadharisha kuwa tayari wameandaa mpango mbadala iwapo Ugiriki itaondoka kutoka kwa Jumuiya hiyo.