Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari,amewafuta kazi wakuu wa jeshi la angani,wanamaji na nchi kavu.
Inaaminika
kuwa rais huyo mpya wa Nigeria amewatimua maafisa hao wakuu jeshini kwa
'kushindwa' kukabiliana na kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Hatua
hii haikuwashangaza wachanganuzi wa maswala ya kiusalama nchini humo
kwani rais Buhari ambaye mwenyewe ni jenerali mstaafu alikuwa ameahidi
wapiga kura katika uchaguzi mkuu uliopita kuwa ataitokomeza kabisa
kundi hilo la Boko Haram.
Habari hii ya kutimuliwa wakuu imetangazwa siku chache tu baada ya mkuu wa jeshi Jenerali Kenneth Minima kusema kuwa
''ongezeko la mashambulizi yanayoshuhudiwa nchini yanalenga kuwatisha wanajeshi ambao yamkini wamewabana Boko Haram''
Jenerali
huyo alisema kuwa kundi hilo limeanza kushambulia watu walioko sokoni
na katika majumba ya ibada kwani wameshindwa kupambana na wanajeshi.