
Takriban milipuko mitano iliyotokea
katika ukanda wa Gaza imeharibu magari ya wanachama wa kundi la Hamas na
makundi mengine ya Jihad.
Haijabainika ni nani alihusika na mashambuli hayo.
Lakini wadadisi wanasema kuwa huenda ni makundi madogo yanayolipinga kundi la hamas ndiyo yaliotekeleza mashambulizi hayo.
Shambulizi
hilo lilifanyika kwenye mtaa mmoja katika mji wa Gaza ambapo vikosi vya
Hamas hivi majuzi vilimuua mwanamgambo aliyeunga mkono kundi la Islamic
State.