Ripoti
kutoka kaskazini mwa Syria, zinasema kuwa wapiganaji wa Islamic State,
wametumia gesi ya sumu kushambulia askari wa Ki-kurd.
Wanaharakati
wanaochunguza vita vya Syria, Wakurd na wenye makao Uingereza wanasema
hayo yalitokea mwisho wa mwezi uliopita,katika mji wa Hasakeh.
Wanasema kuwa makombora yasiyokuwa ya kiufundi, yalitoa gesi ya manjano, iliyonuka vibaya.
Waliokuwako karibu walisikia kichefuchefu, na waliwashwa macho na koo.
Lakini hakuna mtu aliyeumia vibaya.
Maafisa
wa Kikurd wanasema hawajui gesi hiyo ilikuwa ya aina gani, lakini
wanaishutumu IS, kuwa siku za nyuma, ilitumia gesi ya chlorine kama
silaha